Halmashauri ya manispaa ya Ilala kupitia kikao chake cha Baraza
cha tarehe 12/9/2014 imepiga marufuku vitendo vinavyofanywa na halmashauri ya
jiji la Dar es salaam na mawakala wake wa Tambaza auction mart na askari wa
jeshi la polisi kuwakamata wananchi wenye magari ya mizigo ya chini ya tani
tatu na robo na kuwakatia vibali vya shilingi 500,000 kwa mwaka kinyume cha
sheria.
Akisoma tamko hilo, mstaiki meya wa manispaa ya ilala Mhe.Jerry
Silaa amesema halmashauri ya manispaa ya Ilala ndio yenye ardhi na sheria ndogo
ya barabara inayoruhusu magari ya mizigo yasiyozidi tani tatu na robo kuingia
mjini bila usumbufu wowote. Kitendo cha halmashauri ya jiji kutumia sheria
ndogo za iliyokuwa tume ya jiji ambayo wanajua wazi ilivunjwa ni kuwaibia na
kuwanyanyasa wananchi na kuwanyima kufanya shughuli zao za kiuchumi.
Baraza la madiwani linamtaka IGP ernest Mangu awaagize mara moja
askari wake waache kushirikiana na mawakala kuwanyanyasa wananchi kwa kutumia
sheria zilizofutwa na kubaka eneo la utawala la halmshauri ya manispaa ya
ilala. Na aagize vituo vyake vya polisi kutotumika kuwaweka rumande wananchi
bila msingi wa sheria.
Vilevile halmashauri inamtaka msajili wa mahakama kuiagiza
mahakama ya jiji kutotumika kuwatoza faini wananchi na wakati mwengine kuwaweka
rumande.
Halmashauri ya Manispaa
ya Ilala inawataka wananchi waendelee kuzingatia sheria ndogo ya barabara ya
halmashauri ya manispaa ya Ilala na wanapokamatwa na mtu yeyote wadai
kuonyeshwa sheria inayotumika au kufika ofisi ya mkurugenzi wa halamshauri ya
manispaa ya Ilala kwa ufafanuzi zaidi.
Safi sana wamezidi kutunyanyasa.
JibuFuta