Halina mada


TANGAZO
 
UKAGUZI WA MAJENGO NDANI YA MANISPAA YA ILALA
 

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA ANAWATANGAZIA WAMILIKI WOTE WA MAJENGO KUWA, HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA INATARAJIA KUFANYA UKAGUZI MAALUMU WA MAJENGO YANAYOENDELEA KUJENGWA NA AMBAYO YAMEJENGWA KUANZIA MWAKA 2004 NA KUKAMILIKA SASA.

 
KUTOKANA NA UKAGUZI HUO WA MAJENGO, HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA INAWATAKA WAMILIKI WOTE WA MAJENGO KUANDAA NYARAKA MUHIMU ZILIZOKUWA ZIKITUMIKA WAKATI WA UJENZI. NYARAKA HIZO NI PAMOJA JA:-

1.      KIBALI CHA UJENZI KILICHOTOLEWA NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA

2.      MICHORO YOTE ILIYOIDHINISHWA NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA NA KUTUMIKA WAKATI WA UJENZI.

3.      FOMU ZA UKAGUZI WAKATI WA UJENZI PAMOJA NA VITABU VYA MAELEKEZO YA WATAALAM WAHANDISI WAKATI WA UJENZI.

4.      HATI YA KUHAMIA KWENYE JENGO ILIYOTOLEWA NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA.

5.      NYARAKA ZINGINE MUHIMU.

 

LIMETOLEWA:

 

Mashauri Musimu

KAIMU MKURUGENZI WA MANISPAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA   
       
 
 

 
 

 

 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi