Na: Hashim Jumbe
Mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam, Mhe. Paul Makonda leo ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi unaoendelea wa Hospitali ya Mama na Mtoto iliyopo Chanika, Manispaa ya Ilala. Lengo la ujenzi huo ni kuhakikisha Manispaa ya Ilala inakuwa na Hospitali yenye uwezo wa kutoa huduma bora ikiwemo huduma ya upasuaji na maboresho ya huduma ya Mama na Mtoto.
Ujenzi huo unaofadhiliwa na Serikali ya Watu wa Korea Kusini (KOICA) ulianza Februari Mosi,2016 chini ya Mkandarasi aitwaye 'China Hunan Engineering Construction Company' na unategemea kukamilika ndani ya miezi 12, na gharama zake ni Dola za Kimarekani Milioni 4 sawa na Tshs. Bilioni 8.8 za Kitanzania.
Akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi huo, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Dr. Victorina Ludovick alisema "Ujenzi wa Hospitali hii utasaidia kusogeza huduma muhimu karibu na Wananchi wapatao 398,882 kutoka maeneo ya kata ya Chanika, Msongola, Zingiziwa na Majohe na hivyo kupunguza muda na gharama ambazo Wananchi wamekuwa wakitumia kufuata huduma hizo umbali wa kilomita 30 kwenda Hospitali ya rufaa ya Mkoa ya Amana na hivyo kupunguza msongamano"
Akiwahutubia Wananchi waliojitokeza kwenye shughuli hiyo ya uwekaji jiwe la msingi wa Hospitali ya Chanika, Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam, Mhe. Paul Makonda, aliwaasa Wananchi wote watakaonufaika na huduma hiyo ya Hospitali ya Mama na Mtoto kuilinda na kuitunza Hospitali hiyo na miundo mbinu yote itakayokuwepo Hospitalini hapo, Mhe. Makonda alisema "ahadi yangu kama Mkuu wa Mkoa ni kuleta gari ya kubebea Wagonjwa ifikapo mwaka 2017, lakini pia niwaombe tuilinde miundombinu yote itakayokuwepo Hospitalini hapa, na tuamini Hospitali hii ni ya kwetu wote na itahudumia bila kujali itikadi ya chama"

Mchoro wa Hospitali wa Hospitali ya Chanika itakayotoa huduma ya Mama na Mtoto |
Sehemu ya majengo ya Hospitali ya Chanika itakayotoa huduma ya Mama na Mtoto |
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Dr. Victorina Ludovick akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam Mhe. Paul Makonda taarifa ya ujenzi wa Hospitali ya Chanika |
Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Bw. Geum-young Song akitoa neno la salamu kwa niaba ya Watu wa Korea Kusini |
Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam, Mhe. Paul Makonda akiongea na Wananchi wa Chanika wakati wa kuweka jiwe la msingi kwenye Hospitali ya Chanika |
Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam, Mhe. Paul Makonda akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Hospitali ya Chanika, wa kwanza kushoto ni Makamu wa Rais wa KOICA, Bw. Taemyon Kwon |