Na: Hashim Jumbe
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Raymond Mushi leo
amekabidhi mapipa ya kuwekea taka ‘dust
bins’ yaliyotolewa na Umoja wa Wafanyabiashara wa Kariakoo kwa ajili ya
utekelezji wa usafi kwa maeneo ya Kariakoo na Kata zilizojirani na Kariakoo.
Vifaa hivyo, ni ahadi ya Wafanyabiashara hao kwa Mkuu wa
Wilaya ambapo waliahidi kutoa mapipa ya kuwekea taka 60 lakini wameanza na
mapipa 30 ambapo yatawekwa kwenye viunga vya barabara ya Msimbazi ambayo ipo
upande wa Kariakoo na Mchikichini.
Kata nyengine jirani na Kariakoo zitakazonufaika na ugawaji huo
wa mapipa ya kuwekea taka ni pamoja na Kata ya Jangwani na Gerezani.
Aidha, akiongea wakati wa makabidhiano hayo ya vifaa vya
usafi Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bwana Isaya Mngurumi alitoa rai kwa Wafanyabiashara
ndogondogo wanaopanga biashara zao
kwenye barabara ya Msimbazi kuacha mara moja, kwani biashara hizo zimekuwa
usumbufu kwa Watu wanaotembea kwa miguu