WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA MASHARIKI

Na: David Langa, kutokea Morogoro

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa leo amefungua rasmi maonesho ya Wakulima na Wafugaji-Nane Nane kwa Halmashauri zilizopo Kanda ya Mashariki ambazo ni kutoka Mikoa ya Dar-es-Salaam, Pwani, Tanga na Morogoro, ambapo maonesho hayo yanafanyika Mkoani Morogoro na kilele chake ni tarehe 8 Agosti.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni nguzo ya maendeleo: Vijana shiriki kikamilifu ("Hapa Kazi TU")


Waziri Mkuu,Mhe. Kassim Majaliwa wa tatu kutoka kulia akizindua banda la maonesho ya nane nane la Manispaa ya Temeke       


 

Afisa Uvuvi wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Msongo Songoro wa kwanza upande wa kulia akitoa elimu ya upandikishaji samaki kwa njia za kisasa. Wa pili kutokea kushoto ni Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Mhe. Charles Kuyeko




Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sofia Mjema akisalimiana na Watendaji wa Manispaa ya Ilala alipotembelea banda la Manispaa ya Ilala





1 Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi