Na
Neema Lukali
Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2021,
Luteni Josephine Paul Mwambashi ameweka jiwe ka msingi katika mradi wa ujenzi
wa Hospitali binafsi ya Al-Amal iliyopo Kata ya Liwiti Mtaa wa Mfaume wakati
wakikimbiza Mwenge wa Uhuru, Wilaya ya Ilala, tarehe 18 Agosti 2021.
Akisoma taarifa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru, Dkt. Adam Othman ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa ‘DIRECT AID SOCIETY’ alieleza
kuwa mradi huo upo chini ya Asasi ya ‘Direct aid society’ inayojulikana kama ‘AFRICAN
MUSLIM AGENCY’ ambayo ilianzishwa mwaka
1981 na Hayati Dkt. Abdul-rahman Asumer, lengo likiwa kutoa huduma katika
nyanja mbalimbali kama vile; Elimu, Ustawi wa Jamii, Kuyajengea uwezo makundi
maalum pamoja na utoaji wa maji safi, na vilevile Taasisi hiyo imelenga kuchangia
maendeleo ya Afrika katika kutoa misaada ya kibinadam kwa Wanawake, Vijana na
Makundi maalum.
Aidha, Dkt Adam alielezea jinsi mradi huo umeguswa na
kipengele cha nne nukta mbili (4.2) kinachohusika na uwekezaji Wilayani katika
suala zima la afya “Mradi huu wa ujenzi wa hospitali ulianzishwa Juni, 2020 na
unatarajiwa kumalizika Disemba 2021 mpaka hapa uliopofikia, mradi umegharimu
takribani Shilingi Bilioni Kumi na Moja (11) utakapokamilika gharama itafikia
Shilingi Bilioni Ishirini na Nane (28) kwa mahesabu ya ujenzi, vifaa tiba na
thamani”
Kukamilika kwa ujenzi wa hospitali hii utaleta manufaa
zaidi kwa wakazi wa Wilaya ya Ilala na hata walioko maeneo ya jirani.
Hospitali hii itatoa huduma ya wagonjwa
wa nje (OPD) na huduma za ndani, Huduma za Baba, Mama na Mtoto (RCH) vilevile
kutakuwa na huduma za Maabara na Dawa, Huduma za kujifungua kwa wamama wajawazito
pamoja na waangalizi wa watoto wachanga, Huduma za miyonzi kama vile
Ultrasound, X-ray, MRI na CT scan. Pia kutakuwa na uwepo wa madaktari bingwa wa
upasuaji mdogo na mkubwa pamoja na Madaktari bingwa wa meno.
Naye Bwana Ignas Maembe, Afisa Mtendaji wa Kata ya
Liwiti ameupongeza na kushukuru kuwepo kwa mradi huu wa ujenzi wa
hospitali ya Al-Amal uliofadhiliwa
na AFRICAN MUSLIM AGENCY "mradii huu unamanufaa
makubwa sana ya baadaye tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita ikishirikiana na
ufadhili wa ASAS ya AFRICAN MUSLIM AGENCY
kwani utarahisisha watu kupata huduma ya afya asilimia mia moja bila
kwenda mbali na pia mradi huu utaleta maendeleo ya kibiashara katika jimbo la
Segerea".